Kwanza ningetaka kutoa pongezi kwako na jamii yako pamoja na
muungano wa Jubilee, kufuatia uchanguzi wa hapo Machi. Maombi yangu ni kwamba
Mungu atakuongoza unapowajibika katika
utumishi wa taifa letu tukufu.
Kabla sijaendelea ningetaka kujitambulisha. Natoka katika tarafa
moja ndogo wilayani Murang’a kaskazini
katika mkoa wa kati. Mimi ni
mmoja kati ya watoto sita. Baba yangu aliaga dunia tungali wachanga na hivyo
mamangu mzazi kawachiwa jukumu ngumu la malezi. Hali ya uchumi pamoja na
upataji wa lisho la kila siku kwa jamii
nyingi kutoka eneo hili yaendelea kuwa ngumu siku baada ya siku.
Kilimo
ambacho kimekuwa tegemeo letu hakitoshelezi mahitaji yetu. Ukulima wa kahawa
ulianguka miaka mingi iliopita, na sisi kama wakulima wadogo twashindwa tufanyeje. Hali ya anga haiwezi kutegemewa tena, bei ya
mbolea yaendelea kupanda kila kuchao. Muungano wa wakulima wakutetea haki zetu ulianguka
pia kwa hivyo hatuna mtetezi tena.
Kiwango cha
utabibu pia kimepungua. Twazidi kutembea safári ndefu ilikuweza kupokea matibu
na bado gharama yake ni ya hali ya juu sana. Tufanje? Magojwa yenye tiba yazidi
tutuangamiza.
Usafiri na
pia usalama wa kila mmoja wetu bado unatatanisha.
Pongezi kwa
serikali yako kufatia sera za mtangulizi wako kwakuweka mikakati ya kukabiliana
na mambo haya lakini na shindwa kama moja zapo ni za nia njema. Kwa mfano najua
ulituahidi talaklishi lakini nashangaa inahaja gani kwangu kama sina stima,
chakula, hali njema ya elimu na matibabu
karibu nami.
Ombi langu
mtukufu ni kwamba unaweza bado kugairi
nia ilituweze kwanza kutosheleza mahitaji muhimu ya kila mwanachi. Kwanza
tuzidi kunjenga barabara, tuongeze idadi ya waalimu shuleni, tupigane na ukimwi
na tumalize magojwa yenye tiba na pia toboreshe lisho kwa minajili ya jamii
zetu!
Wako Mwananchi Mwaminifu
No comments:
Post a Comment