Sunday 11 August 2013

An open letter to His Excellency President Kenyatta



Kwanza ningetaka kutoa pongezi kwako na jamii yako pamoja na muungano wa Jubilee, kufuatia uchanguzi wa hapo Machi. Maombi yangu ni kwamba Mungu atakuongoza  unapowajibika katika utumishi wa taifa letu tukufu.

Kabla sijaendelea ningetaka kujitambulisha. Natoka katika tarafa moja ndogo wilayani Murang’a  kaskazini katika mkoa wa kati. Mimi ni mmoja kati ya watoto sita. Baba yangu aliaga dunia tungali wachanga na hivyo mamangu mzazi kawachiwa jukumu ngumu la malezi. Hali ya uchumi pamoja na upataji wa  lisho la kila siku kwa jamii nyingi kutoka eneo hili yaendelea kuwa ngumu siku baada ya siku.

Kilimo ambacho kimekuwa tegemeo letu hakitoshelezi mahitaji yetu. Ukulima wa kahawa ulianguka miaka mingi iliopita, na sisi kama wakulima wadogo  twashindwa tufanyeje.  Hali ya anga haiwezi kutegemewa tena, bei ya mbolea yaendelea kupanda kila kuchao. Muungano wa wakulima wakutetea haki zetu ulianguka pia kwa hivyo hatuna mtetezi tena.

Kiwango cha utabibu pia kimepungua. Twazidi kutembea safári ndefu ilikuweza kupokea matibu na bado gharama yake ni ya hali ya juu sana. Tufanje? Magojwa yenye tiba yazidi tutuangamiza.

Usafiri na pia usalama wa kila mmoja wetu bado unatatanisha.

Pongezi kwa serikali yako kufatia sera za mtangulizi wako kwakuweka mikakati ya kukabiliana na mambo haya lakini na shindwa kama moja zapo ni za nia njema. Kwa mfano najua ulituahidi talaklishi lakini nashangaa inahaja gani kwangu kama sina stima, chakula, hali njema ya elimu na matibabu  karibu nami.

Ombi langu mtukufu  ni kwamba unaweza bado kugairi nia ilituweze kwanza kutosheleza mahitaji muhimu ya kila mwanachi. Kwanza tuzidi kunjenga barabara, tuongeze idadi ya waalimu shuleni, tupigane na ukimwi na tumalize magojwa yenye tiba na pia toboreshe lisho kwa minajili ya jamii zetu!

Wako Mwananchi Mwaminifu


No comments:

Post a Comment